Sunday, August 25, 2019

WHAT SHOULD BE DONE WHEN THE COURTSHIP IS BROKEN?

By Pastor Kazi 

Shalom! Shalom!

✍Hebu kwa utulivu kabisa jaribu kufuatana nami hatua kwa hatua katika somo hili sasa. Nina uhakika litakuvusha.

✍Leo kuna vijana wengi wanapata taabu sana katika eneo la mahusiano na wengine kufikia hatua yakudhani huwakupangiwa kuoa au kuolewa. Hapana usikate tamaa tumaini bado lipo.

Lakini pia hata baadhi ya ndoa zinapita kwenye misukosuko mikubwa hata wao wenyewe wanashangaa tatizo hasa ni nini🤷‍♂🤷‍♂🤷‍♂

➡ Uchumba ni kivuli cha ndoa.

➡ Ikumbukwe wazi kuwa Katika Biblia hakuna neno mchumba bali inatumia neno mke.

Tazama kisa cha wachumba hawa Yusufu na Mariam _ biblia inawaita mke na huku hawajafunga ndoa waka Yusufu hajamwonja Miriam. 

*MATHAYO 1:20*

Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

But when he thought about these things, behold, an angel of the Lord appeared to him in a dream, saying, `Joseph, son of David, don`t be afraid to take to yourself Mary, your wife, for that which is conceived in her is of the Holy Spirit.

Kwa nini aitwe mke⁉

🤔 *Kitendo cha kumtamkia binti kuwa unataka awe mke wako. Tayari kwenye ulimwengu wa roho wanarekodi kuwa huyo tayari ni mke wako* ; hata kama ikatokea uchumba kuvunjika bado mbingu zinatambua huyo ni mke au mume wako.

✍Maneno yale ya mahaba mnayotamkiana muwapo wachumba husimama kama *AGANO LA MANENO* linanalo leta muunganiko wa NAFSI mbili pamoja na kuzaa *kIfungo kiitwacho MUUNGANIKO WA NAFSI _ SOUL TIE* na ikitokea sasa mtu hujui namna yakujinasua kwenye hicho kifungo hata kama atakuwa ameokoka bado atateswa na hicho kifungo cha nafsi maana kinachookoka ni roho ya mtu.

🙆🏻‍♂Mbaya zaidi kunawengine wawapo wachumba hushiriki tendo la ndoa; hiyo ni laana kwenye uzao wako bila kuishughulikia mapema itakitesa kizazi chako maana maji hufuata mkondo. Ngono nayo ni Agano linaloachikia kufungo pia cha NAFSI. 

🤔Maana kama tu kumtazama mwanamke kwakumtamani umekwisha kuzini naye sembuse wachumba wanatamkiana na kuapizana hata wengine kuweka agano la damu na kushiriki chakula pamoja. 

*MATHAYO 5:28*

lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

but I tell you that everyone who gazes at a woman to lust after her has committed adultery with her already in his heart.

⏺ Jambo kuu katika somo hili lakilijua tangu sasa; vijana wote uliowahi kuwatamkia kuwa utaoana nao au mkashiriki tendo la ndoa nakisha uchumba huo ukavunjika bado hauko salama kama hujashughulikia hayo maagano Kati yako na hao wachumba na hata ikitokea umeingia kwenye ndoa bado nafsi za hao wanaume au wanawake zitaitesa ndoa yako mpaka ukome. Kufa huta kufa ila chamoto utakipata. Uponyaji wake vunja misingi yote ya uchumba uliovunjika kwa damu ya Yesu na kufanya maombi ya toba na rehema ukiona bado muone kuhani wa Mungu ili akupe ushauri na kuachilia matamuko ya kikuhani kwako.
⏺Tazama kisa cha huyu mwanamke msamaria kahaba kwenye kisima cha Yakobo akiwa na Yesu.

*YOHANA 4:18.*

kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli.

for you have had five husbands; and he whom you now have is not your husband. This you have said truly.`

👆👆Siyo kwamba haowaume watano aliokuwa nao walikuwa nyumbani lahasha! Hii ni lugha ya ufundi_ technical language ikimaanisha kuwa kila mwaume au mwanamke unaye fanya naye tendo la ndoa ni mke / mume wako kwenye ulimwengu wa roho. 

🤔 *Na hii ndiyo moja ya sababu ya jini mahaba* unaota ukifanya tendo la ndoa.

✍NINI KIFANYIKE SASA UCHUMBA UVUNJIKAPO? 

1. TUBU KAMA DHAMBI ZINGINE TU.
✍toba hurudisha ushirika na Mungu.

2. FANYA MAOMBI YA REHEMA
✍Maombi ya Rehema hurudisha uhusiano na Mungu.

3. TANGAZA MSAMAHA KWA YULE ALIYEKUACHA.

4. MSHUKURU MUNGU AMEKUPONYA N.A. MSIBA _ MATESO KWENYE NDOA. 
✍maana ni hatari kuishi na mtu unayempenda atakutesa mpaka ukome ila kufurahisha kuishi na mnayependana 😀😀😀

5. USIFANYE HARAKA KUINGIA KWENYEMAHUSIANO MAPYA
✍jipe muda utulivu na kuangalia wapi ulikosea. 

6. TAFUTA WANANDOA ULIO HURU KWAO WATAKAO KUWA WALEZI NA WASHAURI WAKO WAKUU
✍siyo kila mtu atakushauri vizuri.

7. INUA KIWANGO CHAKO CHA IBADA MBELE ZA MUNGU. 

*MATHAYO 6:33*

...Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na hayo mengine utazidishiwa...

8. TEMBEA UKIJUA KUWA WEWE NI JIBU LA MTU.
✍usijenee maneno ya kipimbavu yatakuchelewa kwenye mema yako.

❤ Mungu akubariki sana ❤
Kwa ushauri juu ya Swala la mahusiano karibu sana.

By Pastor Kazi
Kama umebarikiwa na mafundisho haya, usisite kutoa maoni yako hapo chini sehemu iliyoandikwa "post a comment"

If you are blessed post your comments by pressing on the words writen "post a comment" below.

Also, for advice, advertising, sending us Biblical teachings or Gospel videos or other inquiries, and keep learning the Word of God from all around the world, don't hesitate to contact and keep in touch with Tanzania Gospel Network at: 

Email: tanzaniagospel@yahoo.com, 

Phone no: +255717250805 (Call/Sms/WhatsApp) 

WEBSITE/BLOG: www.tanzaniagospel.blogspot.com

FACEBOOK PAGE
www.facebook.com/tanzaniagospel/ 

ON INSTAGRAM
www.instagram.com/tanzaniagospel/

YOUTUBE CHANNEL
Tanzania Gospel Network


HASHTAG #tanzaniagospel

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed