Monday, March 23, 2015

GEORGE SILAA, MWANAMUZIKI WA GOSPEL HIP HOP

GEORGE SILAA

George Silaa ni mmoja kati ya vijana wanaomtumikia Mungu katika nchi ya Tanzania kwa njia ya Uimbaji wa Muziki wa Injili katika miondoko ya Hip hop. Baadhi ya vijana wengine wanaotumika katika nyanja ya Gospel Hip hop ni Bashando Shaboka, Moses Michael na Rungu la Yesu. George ni Mwanaharakati mzuri katika kuhakikisha vijana wengi zaidi wanaifikia Injili ya kweli na kuwa wanafunzi wa Yesu kama alivyo yeye mwenyewe.


Katika mahojiano na Blogu yetu ya Tanzania Gospel Network, George amefunguka kama ifuatavyo:

Tanzania Gospel Network: George Silaa ni nani hasa
George: George Silaa ni mwanamuziki wa Gospel rap kutoka Moshi, Mkoani Kilimanjaro katika nchi ya Tanzania

Tanzania Gospel Network: Unafanya huduma ngapi katika utumishi wa Kristo
George: Katika utumishi wangu nafanya huduma moja tu ya uimbaji

Tanzania Gospel Network: Niambie kuhusu huduma yako ya uimbaji
George: Huduma hii ni ya Kiinjili kabisa ila ipo katika mahadhi ya Hip hop...so tunaiita Gospel hip hop

Tanzania Gospel Network: Unadhani wajibu mkubwa wa kiongozi wa sifa na kuabudu katika kanisa ni nini?
George: Wajibu mkubwa wa Kiongozi wa Sifa na Kuabudu ni kuwaongoza Wakristo katika kuutafuta uso wa Bwana

Tanzania Gospel Network: Tuambie kuhusu project yoyote unayouifanya sasa hivi; Kiutumishi na katika kujipatia mahitaji yako
George: Katika project zangu zote sio mahali ninapojipatia mahitaji ila malengo yangu ni kwamba kila kijana aisikie Injili ya Yesu. Sasa hivi tuna project kubwa ya Tanzania inayoitwa Yesu Okoa Mitaa maalumu kabisa kwa wana Gospel rap.

Baada ya mahojiano Tanzania Gospel Network ilimshukuru George kwa ushirikiano aliouonesha na kumtakia siku njema.

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed