Thursday, September 25, 2014

MAHOJIANO: MARTIN "BASHANDO" PETER SHABOKA -NASONGA MBELEBashando Peter Shaboka ni moja kati ya vijana wachache nchini Tanzania wanaomtumikia Mungu kwa kuimba Gospel Hip Hop. Baadhi ya wengine ni Moses Michael na Rungu la Yesu. Ni manaharakati mzuri katika Injili ya mitaani kwa lengo la kuwafikia wanajamii hususani vijana, kwani Hip Hop ni mziki unaopendwa sana na vijana.

Katika mahojiano yake leo na blog ya Tanzania Gospel Network, Shaboka, kijana mwenye umri wa miaka 30, anatueleza maisha yake ya kihuduma na harakati mbalimbali katika kuwafikia watu wanaohitaji mguso wa Neno la Mungu katika maisha yao.

Bashando ambaye alipewa jina hilo kanisani baada ya kuwa ananena kwa lugha akitamka neno "bashando", ana kipaji cha kuchora ambapo amewahi kuchorea magazeti mbalimbali yakiwemo Risasi, Mtandao, Kiongozi, na Habari njema lililokuwa linamilikiwa na Bishop Boaz Solo.

Bashando anaamini kuwa haijalishi upinzani anaoupata katika kumtumikia Mungu, yeye atasonga mbele akimtanguliza Mungu siku zote, kwani yeye ndiye mweza wa yote.

Mahojiano naye yalikuwa kama ifuatavyo:

Tanzania Gospel Network: Bashando Peter Shaboka ni nani hasa?

Bashando Peter Shaboka: Jina langu halisi ni Martin Peter Shaboka, hili jina la Bashando ni a.k.a. ambayo imeonekana kuwa na nguvu sana. Niliipata kanisani na imetokana na kunena kwa lugha. Hivyo Bashando ni Mhubiri wa Injili na Mwinjilisti anayetumia nyimbo za mahadhi ya hip hop kulionya kanisa pamoja na watu wengine pale wanapotenda tofauti na Neno.

Tanzania Gospel Network: Unafanya huduma ngapi katika utumishi wa Kristo? 

Bashando Peter Shaboka: Mimi ni Mwimbaji wa hip hop pia ni Mhubiri. 
Tanzania Gospel Network: Niambie kuhusu huduma yako ya uimbaji 
  
Bashando Peter Shaboka: Huduma yangu ya uimbaji naithamini na niaipenda sana, na Mungu kanionyesha makubwa mno kupitia huduma hii. Ikifika wakati wake nitakuwa huru kuyasema, ila zaidi ya yote nitafika mbali sana kihuduma, na maisha ninayoishi ndio Mungu kaniambia niishi hivyo. 

Tanzania Gospel Network: Unadhani wajibu mkubwa wa kiongozi wa sifa na kuabudu katika kanisa ni nini? 

Bashando Peter Shaboka: Muziki ni sehemu ya ibada, na katika saikolojia ya muziki inasemekana hata miti na viumbe vingine huwa vinaenjoy muziki sana, kwa kuwa ni sehemu ya maisha ambayo Mungu ametuumbia wanadamu.Muziki ni sehemu ya maisha na ni kitu kinachokamata hisia; hivyo Kiongozi wa Sifa kazi yake nikuwafanya watu hisia zao zimuelekee Mungu ili waweze kupokea toka kwake kirahisi. 

Tanzania Gospel Network: Tuambie kuhusu project ya YESU OKOA MITAA.

Bashando Peter Shaboka: YESU OKOA MITAA ni Project inayowaunganisha vijana wenye vipaji na ndoto za kubadilisha kizazi hiki kwa kuhubiri Injili. Yesu Okoa Mitaa, tuko wengi sana ambapo nikiwataja kwa majina sitaweza kuwamaliza, but inshort yuko Lawrance Mwantimwa ambae ni mwenyekiti wetu, Mlezi wetu Ron Swai (Katibu Mkuu wa T.A.G.), Rungu la Yesu ambaye ndiye mwanzilishi wa maono haya, pamoja na wengine wengi.

Tanzania Gospel Network: Mafanikio gani yamepatikana katika project hiyo hadi sasa?

Bashando Peter Shaboka: Mafanikio tuliyoyapata kwanza ni kufahamiana na watu mbalimbali ambao wanakielewa hiki tunachokifanya. Pia tunamshukuru Mungu katupatia zana ya kazi ambayo ni video camera.

Tanzania Gospel Network: Unatoa ushauri gani kwa Wanamuziki chipukizi wa muziki wa Gospel?

Bashando Peter Shaboka: Wanamuziki chipukizi nawaambia wasikate tamaa, Mungu aliyeianzisha kazi ndani yao ndiye atakayeitimiza.

Tanzania Gospel Network: Kwa kujifurahisha baada ya kazi, unapendelea kufanya nini?

Bashando Peter Shaboka: Baada ya kazi nimekuwa mtu wa kupendelea kuongea na marafiki mbali mbali kwa njia ya mtandao.

Baada ya mahojiano Tanzania Gospel Network ilimshukuru Bashando Peter Shaboka, mwimbaji wa Gospel Hip Hop mwenye albamu inayokwenda kwa jina la "Naongozwa na Roho" na kumtakia baraka za Mungu katika huduma mbalimbbali unazozifanya katika kuujenga mwili wa Kristo.


KAMA UMEBARIKIWA NA MAHOJIANO HAYA, AU UNA SWALI AU MAONI KUHUSU MTUMISHI WA MUNGU BASHANDO PETER SHABOKA, UNAWEZA KUCHANGIA MAONI KATIKA KIBOX CHA KUCHANGIA MAONI HAPO CHINI, KILICHOANDIKWA "ENTER YOUR COMMENT". AU TUMA EMAIL KWA ANWANI YA tanzaniagospel@yahoo.com

KAMA UNAPATA TATIZO KATIKA KUTOA MAONI. SHUKA HADI CHINI KWENYE KISANDUKU KILICHOANDIKWA "ENTER YOR COMMENT", BONYEZA, HALAFU ANDIKA MAONI YAKO, HALAFU SHUKA HADI SEHEMU ILIYOANDIKWA "COMMENT AS", UTABONYEZA KITUFE KILICHOANDIKWA "SELECT PROFILE", HALAFU CHAGUA "ANONYMOUS", KISHA BONYEZA "PUBLISH". HAPO UTAKUWA UMESHATOA MCHANGO WAKO. KUMBUKA NI VYEMA ZAIDI UKATAJA JINA LAKO.

ASANTE NA BWANA NA AKUBARIKI SANA.

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed