Saturday, June 21, 2014

MWIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI DEBORA SAIDI AFARIKI DUNIA

Kilio kimegubika wapenzi na waimbaji wa muziki wa injili nchini, baada ya mwimbaji Deborah Saidi kufariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es salaam ambako alipelekwa kwa matibabu.

Deborah amefariki dunia ikiwa takribani mwezi toka kusikika kwa taarifa za kuumwa kwake na kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Mwananyamala, kutolewa uvimbe mkubwa tumboni ambao kwa muonekano wa kawaida kabla ya upasuaji huo, alionekana kama ana ujauzito.

BWANA NA AWE FARAJA KWA FAMILIA YA PASTOR JOHN SAID, NDUGU, WANAMUZIKI WA INJILI NA WAPENZI WOTE WA MUZIKI WA INJILI KWA UJUMLA.

source: GK

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed