Saturday, June 21, 2014

MWIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI DEBORA SAIDI AFARIKI DUNIA

Kilio kimegubika wapenzi na waimbaji wa muziki wa injili nchini, baada ya mwimbaji Deborah Saidi kufariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es salaam ambako alipelekwa kwa matibabu.

Deborah amefariki dunia ikiwa takribani mwezi toka kusikika kwa taarifa za kuumwa kwake na kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Mwananyamala, kutolewa uvimbe mkubwa tumboni ambao kwa muonekano wa kawaida kabla ya upasuaji huo, alionekana kama ana ujauzito.

BWANA NA AWE FARAJA KWA FAMILIA YA PASTOR JOHN SAID, NDUGU, WANAMUZIKI WA INJILI NA WAPENZI WOTE WA MUZIKI WA INJILI KWA UJUMLA.

source: GK

Thursday, June 19, 2014

JOB VACANCY: ONLINE AUTHOR

REQUIRED:
A CHRISTIAN
COMPUTER LITERATE
AT LEAST FORM SIX LEAVER
DIPLOMA OR DEGREEE WILL BE ADVANTAGE
READY TO WORK AT LEAST 6 HOURS A DAY

ALL QUALIFIED CANDIDATES SHOULD BE READY TO UNDERGO ONE WEEK TRAINING
APPLICATIONS WITH SCANNED COPIES OF CERTIFICATED SHOULD BE SENT TO mkahaya@yahoo.co.uk OR MANAGING DIRECTOR, TANZANIA GOSPEL NETWORK, P.O BOX 2696, DAR ES SALAAM, NOT LATER THAN 5PM ON 30TH JUNE 2014.


Sunday, June 01, 2014

MAMA MZAZI WA ZITTO KABWE AFARIKI DUNIAMbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Kabwe akiwa na mama yake Mama Bi. Shida Salum, enzi za uhai wake. Mhe. Zitto kupitia mtandao wa Twitter amearifu kuwa mama yake amefariki dunia leo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA).Bi Shida Salun,na Mjumbe wa kamati Kuu ya chama cha CHADEMA,aliyekuwa amelazwa chumba cha Wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU),katika Hospitali ya AMI,Masaki jijini Dar,ameaga Dunia.

(http://ccmchama.blogspot.com/)