Tuesday, April 22, 2014

SOCIAL WORK JOB OPPORTUNITIES IN MWANZA

Mwanza Street Connected
Children Support Project
VACANCIES
Railway Children is a UK based development agency delivering support programmes
for children living alone and at risk on the streets across the world.
Following a review of our operations in Mwanza we will be taking on a team of
highly committed staff to deliver support services to children and young people
on the streets in Mwanza and to vulnerable families and communities across the
city.
Key Requirements
You will have the necessary qualifications relevant to the post for which you
are applying. You will most likely have experience of working in a NGO but most
importantly you will have the passion and drive to make a difference to the
lives of children living on the streets.
Application Process
To apply please send a copy of your CV with a covering letter explaining why
you consider yourself suitable for the role. Please include in the subject
heading which post you are applying for.
You will need to demonstrate how your skills and experience meet the
requirements of the job description. The closing date for all applications is
25th April 2014
A full job description and person specification for all positions is available
online at www.railwaychildren.org.uk/jobs
Please send your application to: g.todd@railwaychildren.org.uk
We anticipate a high demand for this post and regret that only
candidates short listed for interview will be contacted.
Location: Mwanza
www.railwaychildren.org.uk
We fight for children
living on the streets
Posts part funded by UK Aid
2 X Social Worker - Family Work.
2 X Social Worker – Community Work
2 X Street Worker – children and youth.
1 X Street Worker – youth.
1 X Educational Link Worker
1 X Agricultural Link Worker
1 X Entrepreneurship Link Worker
1 X Vocational Training Link Worker
1 X Project Accountant
1 X Driver
1 X Admin Assistant

Work with us | Railway Children
Railway Children is currently recruiting.
railwaychildren.org.uk

VHM TEAM WAVAMIWA NA KUIBIWA!

"Tukiwa wa tunaelekea Matombo Morogoro kwajili ya Mission ya VHM Gari dogo Ilisimama na wakashuka watu 3 wakamkamata aliyekuwa ameshika pesa wakachukua pesa zote pamoja na vifaa vingine na alipokuwa anajaribu kutetea pesa wakampiga na chupa ya bia kichwani akapasuka kichwani lakini tunamshukuru Mungu mpasuko haukuwa mkubwa sana. Sasa Timu imekwama tunasubiria neema ye Bwana waendelee na safari ya huko Matombo." PASTOR MITIMINGI

Monday, April 21, 2014

ADVERTISE YOUR BUSINESS AND / OR ORGANISATIONFOR FREE | REACH MILLIONS OF PEOPLE THROUGHOUT THE WORLD

TO ADVERTISE YOUR BUSINESS AND / OR ORGANISATION FOR  FREE CONTACT US ON +255717250805; OR EMAIL TO mkahaya@yahoo.co.uk. "FREE ADVERTISING ON TANZANIA GOSPEL BLOG" SHOULD BE ON THE SUBJECT LINE.DEADLINE FOR FREE ADVERTISING IS THE SEPTEMBER 2014, UNTIL FURTHER NOTICE.
L

MMEA WA MLONGE- "MORINGA OLEIVERA" | UNTIBU MAGONJWA MENGI IKIWEMO TYHOID NA MALARIA SUGU | PIA UNATUMIKA KATIKA TIBA DHIIDI YA UGONJWA HATARI WA UKIMWIUmewahi kuusikia au kuuona mmea uitwao Mlonge? Au kwa lugha ya kilatini "Moringa Oleivera"? Binafsi niliwahi tu kuusikia na kwa bahati nzuri hivi majuzi nilibahatika kuuona. Mmea unaoonekana pichani wenye shina kubwa ndio Mlonge wenyewe kwa mujibu wa aliyenionyesha kwani mimi sikuwahi kuuona kabla.

Mmea huu ni dawa na unaaminika kutibu magonjwa mengi yawasumbuayo binadamu pengine hata na wanyama wengine. Majani yake,matunda yake,magome yake,maua na mizizi hutumika kama dawa, kila sehemu ya mti kwa umuhimu wake.

Inasemekana matunda yake yanatumika kama mboga kwa kukatakata kama kabichi na majani yake pia hutumiwa kama mboga kwa kupika kama mchicha. Majani yake hutibu magonjwa mbalimbali na kuongeza virutubisho vya mwili.

Maganda(magome) ya Mlonge husaidia kusafisha maji(water treatment).

Mizizi hutumika kutibu watu walio na malaria sugu au watu wanaopata homa ya usiku au wanaotiririka sana jasho wakati wa homa. Mizizi hutumika kwa kusaga unga wake na kutumia kijiko cha chai mara tatu kwa siku.

Kwa mujibu wa nilikodesa,mmea huu hutibu magonjwa mengi kama shinikizo la damu,kupooza viungo au kufa ganzi,homa ya matumbo(typhoid),kuwashwa mwili,vidonda vya tumbo,malaria sugu, enia, upele n.k. Ni magonjwa mengi yaliyoorodheshwa hadi na ukimwi. Sasa sijui ilikuwa ni kutaja tu magonjwa yote yaliyopo au vipi,mimi sijui.


Dozi ya Ukimwi.
Kwa mujibu wa desa lililo na maelezo ya mmea wa mlonge, dozi ya ukimwi ni kutumia unga wa majani kijiko cha chai mara tatu kutwa kwa muda wa siku arobaini na tano sawa na wiki sita. Pia mgonjwa anatakiwa kutafuna mbegu tatu mara tatu kwa muda wa siku arobaini na tano sawa na wiki sita.

Unahamasishwa na kushauriwa angalao nyumbani kwako uwe na mashina kadhaa ya mmea huu kwa matumizi yako. 
(http://nderumo.blogspot.com)

KWA MAHITAJI YA MBEGU, UNGA, MIZIZI, MAGOME NA MATUNDA YA MLONGE WASILIANA NA FESTUS KAHAYA KWA NAMBA +255717250805 au Email: mkahaya@yahoo.co.uk

MCHUNGAJI LUSEKELO AZUNGUMZA KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo, Dar es Salaam, Anthony Lusekelo maarufu ‘Mzee wa Upako’ amemtaka Rais Jakaya Kikwete kusitisha mchakato wa Katiba kwa lengo la kunusuru amani ya Taifa.

Lusekelo alisema siyo lazima Katiba Mpya ipatikane mikononi mwa Rais Kikwete kwa kuwa hatua iliyofikiwa kwa sasa ni kubwa, hivyo inaweza kuendelezwa na Rais atakayefuatia mwaka 2015.


Akizungumza jana katika ibada ya Pasaka, Lusekelo alisema hali inayoendelea kwa sasa inajenga hofu na kuwachanganya Watanzania kutokana na hofu ya Uchaguzi Mkuu ujao.

Alisema Bunge la Katiba kwa sasa limekuwa mfano wa klabu ya pombe za kienyeji kutokana na vurugu alizodai kuchangiwa na wajumbe wa CCM.

“Hakuna majadiliano ya kujenga hoja na badala yake tunasikia matusi tu yanarushwa... uamuzi wa Profesa Ibrahim Lipumba kutoka nje ulikuwa ni sahihi. Hata mimi iwapo ningekuwa mjumbe, ningekuwa wa kwanza kutoka,” alisema Lusekelo na kuongeza:

“Kwa hiyo ni vyema mchakato ukasitishwa kwa hatua iliyofikia ili Taifa litulie na wananchi wajiandae kwa Uchaguzi Mkuu ujao.”

(Chanzo Gazeti la Mwananchi Jtatu - 21/04/2014)

Tuesday, April 01, 2014

BIBLICAL TRANSLATION OF NUMBER FOUR | TAFSIRI YA NAMBA 4 KIBIBLIA | BY PASTOR PETER MITIMINGI

Tumeuanza mwezi wa 4. 2014

Namba NNE ni namba ya uumbaji.

1. Katika siku ya NNE Mungu alikamisha kuumba vitu.

2. Kuna pande kuu NNE zinazokamilisha dunia, (Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi (Isa 11:12).

3. Katika Hekalu la Ezekiel kulikuwa na meza za sadaka NNE upande mmoja na NNE upande mwingine.

4. Siku imegawanyika katika sehemu NNE. (Asubuhi, Mchana, Jioni na Usiku).

5. Katika amri kumi, amri NNE zinahusisha zaidi juu ya dunia.

6. Injili NNE zinawakilisha maisha ya Yesu hapa duniani.

7. Wanawake wa-NNE wametajwa katika mlolongo wa kuzaliwa kwa Yesu. (Thamar, Rahabu, Ruth na Mke aliyekuwa wa Huria).

8. Kuna vijana wa-NNE wa-Kiebrania waliotajwa katika kitabu cha Daniel.

9. Kuna wafalme wa-NNE waliotajwa katika kitabu cha Dniel. (Nebukadineza na Belshashaza wa wafalme wa Babeli, wengine ni Dairo na Silas wa Uajemi).

10. Ezekieli inazungumza juu ya Hukumu NNE juu ya Dunia.

11. Vizazi vi NNE vilionwa na Ayubu kabla ya kufa kwake (Job 42:166)

12. Kambi ya waisrael iligawanyika katika sehemu kuu nne Hesabu 2:1-34

13. Baada ya Yesu Kutungikwa msalabani askari wa kirumi waligawanya vazi la Yesu vipande vine kila kipande kwajili ya kila mmoja wao. Yoh. 19:23

14. Kuna vipindi muhimu vinavyo ongoza majira katika dunia.(1. Fall 2. Winter 3. Spring 4. Summer)

15. Siku imegawanyika katika vipindi vine. (1. Asubuhi 2. Mchana 3. Jioni 4. Usiku)

16. Yesu alitoa mfano wa aina nne za Udongo. Mathayo 13.

Namba NNE ni namba ya uumbaji.
Ninamuomba Mungu katika mwezi huu wa 4 Aumbe jambi jipya katika mwezi huu uwe mwezi ambao utauma mafanikio na baraka katika maisha yako


YOU ARE WELCOMED POST YOUR COMMENTS CONCERNING THE LESSON BELOW
UNAKARIBISHWA KUTOA MAONI YAKO KUHUSIANA NA SOMO HAPO CHINI