Thursday, February 20, 2014

DON'T GET MARRIED TO A PERSON BECAUSE YOU WANT TO HELP HIM OR HER OR YOU FEEL SYMPATHY TO HIM OR HER | USIOE AU KUOLEWA KWASABABU YA KUMSAIDIA MTU FULANI AU KUMUONEA HURUMA | by PASTOR MITIMINGI

 Pastor Mitimingi
1. Kuoa au Kuolewa na Mtu kwasababu ya Kumuonea Huruma.
• Kuoa au kuolewa na mtu kwa sababu ya kumuonea huruma ni moja kati ya sababu zisizo sahihi. Na inaonekana kuwa ni sababu moja ya kijinga pia.
•Ndoa zianazo oana kwa misingi ya kumsaidia mtu au kumwonea mtu huruma huwa hazina maisha.

2. Huruma ya Kujiona kuwa ni wewe Ndio Unawajibika.
Getting married to a person for a reason that you are responsible to help him or her is unwise thing
Kumhurumia mtu na kujiona kuwa una wajibu wa kumsaidia ni vizuri, lakini kuolewa naye kwa sababu hiyo ni wazi kuwa ni jambo lisilo la hekima kabisa.

3. Ndoa ni yathamani Kuliko Huruma ya Mahusiano.
Marriage is more precious than relationship-based sympathy
• Ndoa ni kitu cha thamani zaidi kuliko mahusiano ambayo yamejijenga katika huruma.
Chukulia kwamba kama mhusika ana masaa sita tu kuishi baada ya ndoa. Kwa hiyo utaishi katika ujinga huo kwa masaa sita tu maana kinyume na hapo utaishi maisha yako yote ukiwa unajihisi mjinga zaidi na mwenye huzuni.
• Hiyo itakuwa ni sabau ya kuvunjika kwa ndoa hiyo kwa sababu utaonekana mbaya zaidi ya kabla hujaingia.

4. Kuoa au Kuolewa kwajili ya Kumsaidia Mtu Anayeteseka.
Don't get married to a person because you have decided to help that person
If you want to change your partner, do it before marriage and not after marriage
•Usioe au kuolewa na mtu eti kwasababu unaamua kumsaidia kutokana na shida Fulani.
• Mfano kuna baadhi ya watu utakuta mwanaume anaamua kumuoa msichana fulani eti kwasababu kule anakoishi wanamnyanyasa na kumtesa so anaamua amsaidie amuoe ili aishi naye.
• Hii ni sawa na ile ya ujinga wa kufikiri kwamba utaoa au kuolewa na mtu kwa matumaini kwamba utambadilisha mtu baada ya kuolewa au kumuoa ili afanane na wewe, dini yako au tamaduni zako.
• Kumbuka kwamba, kuwa na jitihada za kukubaliana sio kubadilika, sababu suala ndoa halina haja ya kuweka mabadiliko kwa mtu yeyote.
• Ukitaka kumbadilisha mwenzi wako usisubiri kwenda kumbadilishia ndani fanya hayo mabadiliko kabla ya kuingia ndani.
Unakaribishwa kutoa maoni yako kwani tunayathamini | You are warmly welcomed to share your precious comments

Monday, February 17, 2014

KAZI YA MAOMBI YA REHEMA

Mwl: Mwinj & Mch. SONGWA, MM. KAZI

MAANDIKO: Ebr 4:16, Mith 3: 3 – 4, 1 Yhn 3:21-22.

YALIYOMO:
1. Utangulizi
2. Maana ya Rehema na Neema
3. Kazi ya Maombi ya Rehema na matokeo yake
4. Faida ya Maombi ya Rehema
5. Aina ya msaada upatikanao kwa Neema kwa njia ya Maombi ya Rehema

01. UTANGULIZI
Je, umewahi kukaa chini na kujiuliza maana ya maneno haya mawili maarufu sana; yaani Rehema na Neema?
Je, unajua Rehema hushughulika hasa na nini katika maisha ya mwamini? Hali kadhalika na Neema hushughulika na mambo gani katika maisha ya mwamini?
Basi; kwa kuifahamu zaidi fuatana nami katika somo hili. Na Mungu akubariki sana.

02. MAANA YA REHEMA NA NEEMA
I. REHEMA:
- Ni ile hali ya kutopata adhabu unayostahili kabisa kupewa kwa sababu ya uovu, dhambi au makosa yaliyofanywa nyuma.
- Ni msamaha wa mwisho wa Mungu uambatanao na kusitishwa kwa adhabu stahiki
- Ni kutopata unachostahili
- Ni msamaha

KUMBUKA: Kimsingi Maombi ya Rehema ni Toba ya kweli mbele za Mungu dhidi ya uovu, dhambi na makosa yaliyofanyika nyuma, Kut 20: 1 -4.

II. NEEMA:
- Ni kupewa usichostahili
- Ni hali kustahilishwa, kupendezwa, kuhurumiwa na Mungu (Favour and Spiritual Blessings of the Lord Jesus Christ.)
- Kuhesabiwa haki vure ( kazi ya msalaba)

03. KAZI YA MAOMBI YA REHEMA NA MATOKEO YAKE
I. Kazi ya maombi ya Rehema;
(a) Kufuta hati ya mashitaka; hali ya kuondoa uhalali wa shetani kututawala na kukutumikisha, Kol. 2 : 14
Pindi unaporudi kwa Yesu unapewa haki na uweza Yhn 1;12

(b) Kupata Ujasiri mbale za Mungu 1 Yhn 3: 21- 22, Mwanzo 3: 8 – 19.

Tabia za Mtu jasiri
Josh 1:1-9, Sam 17: 8-47, Amuzi 14:6, 19, 15:4, 13, 15, 16:3, 27
- Hana hofu ( Fearless person)
- Ana uhakika, anajiamini, shupavu, ana matumaini ( confident person)
- Ni shujaa, thabiti, jeuri (bold person)
-
Mambo yanayoondoa ujasiri ni; Isaya 59: 1-4
- Uovu, dhambi na makosa yetu.

Kumbuka: Kitu pekee kinachompa kiburi na jeuri shetani cha kututesa na kututawala ni ni uovu, dhambi na makosa yasiyotubiwa, Yhn 8: 34, 42-44
Hivyo Mungu anakusihi utubu ili akurejeshee ujasiri na mamlaka ya kumshinda aduui, Ezek 18: 21- 23.

(c ) Kutupa Kibali mbele za: Mith 3: 3- 4, Lk 2 : 52
- Mungu – Ushirika mzuri na Mungu
- Wanadamu – kusikilizwa, kutambuliwa, kufurahishwa na kuheshimiwa.

Kumbuka:
Mtu anapoteza kibali mbele za Mungu na wanadamu; katika ulimwengu wa roho anakuwa kama mtu aliyepakwa mavi usoni na anatoa harufu chafu ( uvundo). Hata kama mtu ana huduma nzuri , ana karama na vipawa vizuri akipoteza kibali tu, hatakubalika kamwe mpaka atengeneze na Mungu, Malaki 2:3.

Angalizo:
Uwe makini kulinda kibaki- ushirika mzuri na Mungu na wanadamu ili usije ukapakwa mavi usoni – ukapoteza kibali.

(d) Kutupa akili nzuri mbele za ; Mith 3:3-5, 24: 3-9, 1 Kor 15: 33- 34
- Mungu
- Wanadamu
Biblia inasema sana juu ya akili, kuwa Mungu ameruhusu tuzitumie akili lakini siyo kuzitegemea kwani akili zina mwisho wake.

Matunda ya akili nzuri ni; Mith 24: 3-6, 3: 13-20
- Hekima (nguvu), maarifa (elimu).
- Ufahamu (Ujuzi na ustadi)

Kumbuka: Urithi wa mwenye akili ni maarifa kwani ana busara, bali urithi wa mjinga (asiye na akili) ni upumbavu, Mith 14: 18


Jambo la msingi la kuelewa vizuri kati ya Rehema na Neema ni kwamba;
-Rehema kazi yake ni kushughulikia MSINGI wa maisha ya mtu, Zab 11:3, yaani mambo ya nyuma. Yanawezekana mengine huyakumbuki; haya ni pamoja na yote yaliyotendwa na watu wengine pamoja na yale uliyotenda mwenyewe.
-Mambo ya nyuma yana uwezo wa kukukwamisha mbele ya safari hata usiweze kuumaliza mwendo; yaani kuyatimiza malengo na makusudi ya Mungu katika maisha yako.
-Neema kazi yake ni kushughulikia JENGO (Maisha) – 1Kor 3:9- 15, na mambo yajayo Ebr 4: 16 (Tazama pia Yer 1:10, Math 13: 24-30, Math 15:13_)

04. FAIDA YA KUMWENDEA MUNGU KWA MAOMBI YA REHEMA
Ebr 4: 16 na Math 5: 7

Faida ni matunda mazuri ya kitu au jambo.

Zifuatazo ni baadhi ya faida:
(i) Tunapokea Rehema ( Msamaha) kwa yale tuliyoshindwa ( Help for our failures)
(ii) Tunapata Neema ya kutusaidia katika nyakati ngumu za uhitaji, 2 Kor 12 : 9- 10)

05. AINA YA MSAADA UPATIKANAO KWA NEEMA KWA NJIA YA MAOMBI YA REHEMA
Ebr 4: 16
Tunapata:
(i) Msaada ufaao ( appropriate help)
(ii) Msaada ujao kwa muda/ majira/ wakati sahihi kabisa wa Mungu ( Divine well-timed help)

Kumbuka: Toba ya kweli huleta Ufalme wa Mungu kwenye maisha ya mtu, Math 4 :17, 3: 2


UISHI MILELE
2Kor 13;14


IMEANDALIWA NA:
Mwl: Mwinj & Mch. SONGWA, MM. KAZI
SIMU: 0757-567899. 0789-567899. 0719-968160, 0779-597066
Email: songwa@yahoo.com ptrsongwak@gmail.com
TAG KONGOWE FOREST. DSM. P.O. Box 70983. DSM.