Thursday, November 21, 2013

AINA 12 ZA WATU WASUMBUFU KATIKA JAMII BY PASTOR PETER MITIMINGI

 MTU WA TATU
BLANKETI LENYE MAJI

 Pastor Mitimingi akiwa London

1. Hakuna mtu anayeweza kupata usingizi akifunikwa blanketi yenye maji baridi.

2. Blanketi lenye maji, Mtu huyu wakati wote hutazamia mabaya kumpata yeye na wakati mwingine hutazamia mabaya kuwapata watu wengine. Hutafuta mabaya ndani ya mabaya na pia hutafuta mabaya ndani ya mazuri pia.

3. Hujiwazia mabaya yeye mwenyewe na huwawazia mabaya pia watu wengine pia.

4. Ni mtu anayechosha katika uhusiano. Ukihusiana naye kwa muda mfupi tu, unasikia kumchoka. Kama akiwa ni mwenzi wako anakufanya mpaka ndoa unaiona imejaa takataka.

5. Ni mtu wa kuvunja moyo kila anaye kutana naye. Humfunika kila mtu na blanketi lake la maji baridi.

6. Ni mtu ambaye yeye mwenyewe amejikinai na kujichoka. Yeye mwenyewe anajionea kinyaa, sasa unategemea watu wengine atawaonaje?

7. Haamini juu ya jambo jema lolote kutendeka kwake au kwa mtu mwingine. Anawaza mabaya, ananena mabaya na anatenda mabaya kwake na kwa wengine pia.

8. Ni mtu anayekwepa majukumu ya mabadiliko. Hataki kushughulika na mambo yatakayo pelekea mabadiliko yake biafsi. Kukiwa na mafundisho hushabikia wengine wabadilike lakini sio yeye mwenyewe.

9. Amejifunika na blanketi ya maji awezi kupata raha na huondoa raha kwa wengine pia.

10. Hali yake ya Moyo imeharibika kabisa na huharibu hali za mioyo ya wengine.

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed