Saturday, November 02, 2013

AINA 12 ZA WATU WASUMBUFU KATIKA JAMII BY PASTOR PETER MITIMINGIPastor Peter Mitimingi akifundisha vijana katika semina


Utangulizi:

Katika jamii tunayoishi sasa kuna aina na makundi mbalimbali ya watu. Kunawengine ni waungwana sana, wengine wakorofi sana, wenye tabia nzuri na wenye tabia mbaya pia.

• Katika kila watu 10 kuna vichaa 2

• Kuna watu wanakwaza mpaka hautamani kuishi nao

•Hao vichaa 2 wamewekwa maalumu ili kukushughurikia usije ukaota kiburi.


MTU WA KWANZA

MKOSOAJI
1. Mtu huyu Siku zote hudumu kulalamika na kunungunika kwa kila jambo.

2. Huwa haridhishwi na jambo lolote hata ukijitahidi kumtendea mema bado atakosoa tu.

• Usipompa chakula, atalalamika

• Ukimpa chakula atasema umempa chakula kilichopoa.

• Ukimpa chakula cha moto atasema unataka kumuunguza mdomo. Nk.

3. Mara zote hutoa ushauri usiotakiwa au utakaoleta malalamiko kwa wengine pia.

4. Yeye mwenyewe hawezi kufanya lolote jema bali hudumu kulalamika na kukosoa wengine.

5.Hujitahidi sana kusikiliza na kutafutiza makosa tu, huyashika makosa tu na kamwe hana muda wowote wa kushika jema lolote.

6. Yeye mwenyewe hana jibu lolote wala suluhisho mkononi juu ya kile anachokosoa.

7. Ni watu waliojaa unafki watu wenye sura mbili

.......................................ITAENDELEA.............................................

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed