Monday, November 04, 2013

AINA 12 YA WATU WASUMBUFU KATIKA JAMII BY PASTOR P.ETER MITIMINGIVijana wakiwa katika mafundisho


MTU WA PILI
SPONJI
1. Kazi kumbwa ya mtu wa aina hii ya sponji kama unavyojua sponji kazi yake ni kufyonza tu mara inapowekwa kwenya maji huachukua maji kutoka kwenye bakuli na kuyahamishia kwake.

2. Mtu huyu wakati wote ana uhitaji, lakini kamwe hatoi kitu kwako.

3. Ni mtu wanaotumia vitu na mali za watu wengine kwa manufaa yake binafsi na kamwe hawezi kuwaza wala kupenda kutoa vyake kwa wengine.

4. Anataka yeye tu, ndiye wapewe. Asipopewa anakuwa mkali na lawama nyingi na wakati mwingine kususia jambo fulani.

5. Huwa hatoi sadaka wala mafungu ya kumi kanisani wala michango yeyote ya harusi au jumuiya fulani. Neno SINA kwake ndio kama wimbo wa taifa anauimba kila iitwapo leo.

6. Yeye anapokuwa na jambo linalo mhusu, huwa wakwanza kuchangisha na kudai michango hata kama ni kwanguvu atataka achangiwe au asaidiwe tena kwa haraka bila ya kucheleweshwa..

7. Wakati mwingine hudai michango kana kwamba niyeye aliye kukopesha kumbe ni msaada au mchango anadai kwa nguvu na vibaya mpaka inakuwa kero kwa yule anayetaka kumchangia au kumsaidia.

8. Sponji hujihalalishia kwamba yeye ni maskini hivyo anakibali na sababu nzuri za kutokutoa. (Excuses)

9. Sponji Haina Uwezo wa Kutunza Maji Iliyoyanyonya Chomboni
Mara nyingi sponji inaponyona maji kutoka kwenye chombo, ukiitoa nje ya chombo huwa haina uwezo wa kuyatunza yale maji iliyoyanyonya kutoka kwenye chombo na kuyahifadhi, badala yake yale maji hudondoka na kupotea kabisa.

10. Mnyonyaji hana Uwezo wa kutunza alichonyonya kutoka kwa watu
Ndivyo alivyo mtu huyu aina ya Sponji hata kama atapata pesa na mali kwa kunyonya kwa wengine mara nyingi ni watu wasio na maendeleo kabisa kwani huwa hawana uwezo wa kutunza na kumiliki vile walivyoweza kunyonya kutoka kwa wengine.
KAMA UMEBARIKIWA SEMA NIMEBARIKIWA!

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed