Sunday, February 17, 2013

TOBA YA KWELI

Na Mch. Maghembe 17 Feb 2013

TOBA

Ni kusikitikia na kujutia dhambi kiasi cha kuiacha kabisa.

Toba ya kweli inamhusisha mtu mzima mzima.

PEMBETATU YA TOBA

Toba ya kweli inahusisha vitu muhimu vitatu ambavyo ni:

i. Akili

ii. Hisia

iii. Utashi

I. AKILI
 Toba ya kweli ni lazima ihusishe akili ambapo mtu ni lazima:
  • Atambue kwamba amemkosea Mungu
  • Aione dhambi kama Mungu alivyoiona
  • Aitambue Neema ya Mungu iokoayo.

II. HISIA
Mungu anazingatia hisia za mtu ili kubaini toba ya kweli

Mtu anapaswa:
  • Aone aibu kwa kuwa mtenda dhambi
  • Ajisikie vibaya na uchungu

III. UTASHI
Utashi unahusishwa katika toba ya kweli ambapo mtu ni lazima:
  • Ageuke na kubadilika moyoni, tabia na mwenendo.
  • Awe tayari kuchukua gharama kama vile kuacha kazi, mke, mume, ajira n.k


 
Mfano wa toba ya kweli: Luka 15: 11-32
- Habari ya mwana mpotevu

1 comment:

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed