Thursday, January 03, 2013

SAJUKI AFARIKI DUNIA


Sajuki enzi za uhai wake


Msanii wa filamu nchini Tanzania, Juma Kilowoko almaarufu Sajuki, amefariki dunia asubuhi ya jana tarehe 2/1/2013 saa 1:30 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, siku moja baada ya kuuanza mwaka mpya wa 2013. Umauti umemkuta msanii huyo baada ya hali yake kuanza kutengamaa akiwa amesharejea nchini kutoka Indiaalipokuwa anatibiwa maradhi ya saratani. Siku chahe kabla ya kukutwa na umauti, Sajuki alianguka akiwa jukwaani akiwa katika tamasha la kuwashukuru mashabiki wake mjini Arusha na baadaye kukimbizwa Dar es salaam kwa ajili ya matibabu ambapo baadaye aligundulika kuwa na tatizo la upungufu wa damu, lakini hazikupita siku nyingi hadi alipoiaga dunia.

Msiba upo Tabata Bima amabapo mipango ya mazishi inaendelea kufanywa. Mwili wa marehemu Sajuki unatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 4/1/2013 kisukuru Dar es salaam. Marehemu ameacha mjane na mtoto mmoja. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe, amen.(picha kwa hisani ya http://kajunason.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed