Tuesday, January 22, 2013

JINSI YA KUPOKEA MUUJIZA KUTOKA KWA MUNGU (MATHAYO 14:22-33 )


MUUJIZA MKUBWA KUPITA YOTE MUNGU ANAOWEZA KUTUFANYIA NI KUTUPA WOKOVU.
Mathayo. 14:22-33

Kama anaweza kufanya muujiza mkubwa kabisa, miujiza mingine midogo anaweza kuifanya pia; kama vile kutuponya, kutupa baraka za kifedha n.k.

Jinsi ya kupokea muujiza wa kifedha

  • Mwombe Mungu akupe mbegu ya kupanda.
  • Ukishapata mbegu ipande nayo itazaa mia, sitini na thelathini

Vitatu vitatu vya muhimu kuzingatia ili upokee muujiza:

  • Weka ahadi za Mungu (ardhi ngumu) chini ya miguu yako-; simama juu ya ahadi za Mungu na hutazama.
  • Elekeza macho yako kwa Yesu; usipoteze muda wako kwa mambo yasiyofaa.
  • Omba bila kukoma
 

HOW TO RECEIVE MIRACLE FROM GOD (MATHEW. 14:22-33)

The greatest miracle God can do for us is that he can save us.

Math. 14:22-33

If he can do the greatest miracle, the other miracles which are minor he can also do; for example healing, giving us the financial breakthrough etc.

How to receive Financial miracle
  • Ask God to give you seed that you may sow.
  • After getting the seed sow it and you may reap 100, 60 and 30.
Three things important towards receiving miracle:
  • Put God’s promises (solid ground) under your feet; stand on them and you wont sink.
  • Fix your eyes on to Jesus; don’t concentrate on negative things.
  • Don’t give up on your prayer

Thursday, January 03, 2013

SAJUKI AFARIKI DUNIA


Sajuki enzi za uhai wake


Msanii wa filamu nchini Tanzania, Juma Kilowoko almaarufu Sajuki, amefariki dunia asubuhi ya jana tarehe 2/1/2013 saa 1:30 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, siku moja baada ya kuuanza mwaka mpya wa 2013. Umauti umemkuta msanii huyo baada ya hali yake kuanza kutengamaa akiwa amesharejea nchini kutoka Indiaalipokuwa anatibiwa maradhi ya saratani. Siku chahe kabla ya kukutwa na umauti, Sajuki alianguka akiwa jukwaani akiwa katika tamasha la kuwashukuru mashabiki wake mjini Arusha na baadaye kukimbizwa Dar es salaam kwa ajili ya matibabu ambapo baadaye aligundulika kuwa na tatizo la upungufu wa damu, lakini hazikupita siku nyingi hadi alipoiaga dunia.

Msiba upo Tabata Bima amabapo mipango ya mazishi inaendelea kufanywa. Mwili wa marehemu Sajuki unatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 4/1/2013 kisukuru Dar es salaam. Marehemu ameacha mjane na mtoto mmoja. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe, amen.(picha kwa hisani ya http://kajunason.blogspot.com)

BISHOP MWASOTA AONYA KUHUSU ‘COPY’ KATIKA UKRISTO.Bishop David Mwasota wa kanisa la Naioth Gospel Assembly lililopo mabibo external, Dar es salaam amesema hayo katika ibada ya kuanza mwaka mpya wa 2013 hapo kanisani ambapo washirika wemgi walijitokeza katika madhabahu ya Bwana na kutoa shuhuda kwa mambo Mungu aliyowafanyia kwa mwaka mzima wa 2012.

Akionya katika mahubiri yake alisema kwamba hivi sasa kumezuka imani katika Ukristo ambazo waumini hufanywa kumfikia Mungu kupitia watumishi wanaowaongoza. Watumishi hawa huwafanya waumini wao kuwategemea wao kwa mambo yote ya kiroho hususani suala zima la maombi na hivyo kuwafanya wasiwe na uwezo wa kujitegemea kiroho.

Bishop Mwasota aliweka bayana kuwa hali hii ni ‘copy’ nyingine iliyokuja badala ya imani ile ambayo wengi walikuwa nayo awali kabla ya kuokoka ambapo waumini humwendea Mungu kupitia kwa watumishi. Askofu alisisitiza hili akitolea mfano kwa watumishi wengine wanaosisitiza watu kwenda kwao kuombewa tu pasi na kuwahimiza kufanya mambo mengine yawapasayo kufanya.

Aidha, Askofu Mwasota ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania (PCT), alifanya maombi ya kifamilia kwa washirika wake katika ibada hiyo pamoja na kuombea mafuta ya mizeituni ambayo waumini walikuja nayo ili yawe na upako utakaosambaratisha matatizo na nira katika maisha yao. Askofu ameamua kuweka upako katika mafuta na waumini kuyatumia kupaka kichwani, katika nyumba n.k. baada ya yeye kupata muujiza mkubwa kutokana na mafuta yenye upako.

Mbali na hayo, katika ibada hiyo Mtumishi wa Mungu alitamka baraka kwa washirika ikiwa pamoja na magari na fedha nyingi kwa mwaka 2013. Baada ya yote, siku iliisha kwa kula chakula cha pamoja kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya wa 2013 ambapo watu wa rika zote, wake kwa waume walishiriki katika chakula hicho.


(picha kwa hisani ya blogu ya gospelkitaa)