Thursday, November 29, 2012

NYUMBA NA GARI LA MWIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI NCHINI TANZANIA SAMSON KABATA VYETEKETEA KWA MOTO
Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Samson Kabata, siku ya jana nyumba pamoja na gari yake vimeteketea kwa moto.Nikizungumza na Kabata amesema yeye alikuwa kazini ndipo akapigiwa simu na wapangaji wenzake nyumba inaungua pamoja na gari yake.Kwa mujibu wa Kabata anasema chanzo cha moto kimesababishwa na mpangaji wa jirani yake kuacha pasi ikiwa kwenye umeme kisha ikalipuka. Samson Kabata mwimbaji wa nyimbo za injili. 
Picha na habari kwa hisani ya blogu ya Unclejimmy Temu zimepatikana kutoka katika blogu ya Gospel Kitaa

Sunday, November 25, 2012

MPENDE MUNGU ILI UYAFIKIE MAFANIKIO YA MAISHA YAKO

RUM 8:28

UTANGULIZI
Ahadi hii ni kwa wale tu wampendao Mungu na wajinyenyekeshao kwake kwa njia ya imani katika Kristo (Zab. 37:17).

Mungu anafanya kazi na wale wampendao.

I. SIRI KUBWA YA MAFANIKIO YA MTU NI:
1. Kumpenda Mungu. 
Mungu anafanya kazi na watu manaompenda.
Wale wampendao ndiyo anafanya kazi nao.

Alifanya kazi na Petro ambaye hakusoma akawaacha wasomi makuhani. Miaka 40 kiwete hajawahi kuingia hekaluni akakutana na watu wanaompenda Mungu akapona; angali makuhani wasomi walikuwepo wasiweze kutumiwa kumponya wa huyo kiwete.

2. Ukimpenda- Utajulikana naye (1Kor. 8:3).

Hata kama serikali, balozi n.k. hawakujui lakini wewe unajulikana na Mungu.

Ukijulikana na Mungu matatizo yako yatakuwa bayana, hata kama unapitia mambo magumu, lakini unajulikana mbele zake.

II. UKIMPENDA MUNGU IKO SABABU (2Kor. 3:5-6)

Unatoshelezwa na Mungu.

Hautoshi wewe mwenyewe.

Hautoshi na elimu yako.

Hautoshi na nguvu zako, uwezo wako, Mungu ndiye aingilie kati ndipo utoshelevuwako utatosha.

“TUNATOSHELEZWA NA MUNGU TU”

Adui wakikufuata yeye anajitokeza adui- anakimbia.

“UKIMPENDA MUNGU YEYE ATAKUTOSHELEZA”

Siku zako zitazidishwa (Mit. 9:11).

Hata kama wachawi, wabaya watakutafuta, Baraka zaozitaongezwa; siku zitaongezwa.

Yakatae magonjwa yapeleke kwa wale wanaokuchukia. (Kumb. 7:15)

Utastawi (Zab. 72:7, 92:13b)

Atakuwa na amani (utulivu, uponyaji, uzima, furaha n.k.)

Utazaa matunda (Zab. 92:14)

Utakuwa na ubichi, Bwana atakubariki mpaka uzee wako.

Ibrahimu akiwa na kama miaka 90 ndiyo anazaa, miaka haijalishi mbele za Mungu. Usibabaike kwa miaka mingi kupita.

MUNGU TUNAYEMHUBIRI NI MUHIMU AFANYE MUUJIZA KATIKA UZEE

Tunaye atutimiziaye mambo yetu (MUNGU) “mwite” (Zab. 57:2). Hata kama afya yako imechukuliwa, elimu yako imechukuliwa- Mungu hajabadilika, kama aliokoa, anaokoasasa, kama aliponya ataponya sasa, atabariki.

Utanenepa (Neh. 9:23-25)

Bwana akutishie wenyejiwa nchi hiyo (unakofanya kazi, unakoishi) ndiyo maana wachawi, mapepo tunayatenda kama tupendavyo/ tutakavyo.

Nawe utawatenda wachawina wafuga majini kama utakavyo.

Wakala, wakashiba, wakanenepa. KUNENEPA NI MPANGO WA MUNGU. Bwana akupe kula na kushiba na kunenepa. Funga nzuri ni pale ambapo mtu ana chakula cha kutosha.

Ukimpenda Mungu, atakupa kula na kushiba, kunenepa.
“JIHOJI UNAMPENDA MUNGU?”

Prepared by; Rev. Joseph Marego Mob: +255754334640/ +255712498080

Wednesday, November 21, 2012

UTAKATIFU BINAFSI

JINSI YA KUPATA UTAKATIFU
(1Petro 1:15-16)

Neno “Utakatifu” maana yake halisi ni kutengwa ili utumike katika matumizi maalum ya Kimungu.

Utakatifu unahitaji mtu kutengwa kutoka katika ulimwengu wa kawaida kwenda katika ulimwengu wa utauwa.

I. HATUA TATU ZA UTAKATIFU

i. Hatua ya kwanza ni “Wokovu”

Kutengwa kwa nia ya Mungu (1Kor 1:2)

a) Wazo la “Mahali patakatifu” lilikuwa katika nia ya Mungu.

b) Wakristo wote wametengwa katika nia ya Mungu na ni Watakatifu.

c) Hatua ya kwanza ya Msingi katika Utakatifu wa mtu ni Wokovu kwa kumwamini Bwana Yesu Kristo na ile Dhabihu aliyoitoa.

ii. Hatua ya pili ni “kujitoa”

Kutengwa kwa Mungu katika nia ya Mwamini (Rum. 12:1)

a) Bwana Yesu alitolewa katika nia ya wazazi wake.

b) Wakristo wote wanaweza kujitoa kikamilifu kwa Kristo.

c) Hatua ya pili ya Utakatifu wa mtu ni kuyatoa maisha yake kwa Mungu kwa njia ya shukrani kwa ajili ya upendo wake na rehema.

iii. Hatua ya tatu “kugeuzwa”

Muumini kujitenga kwa ajili ya Mungu katika maisha yake (2Tim. 2:19-22, Efeso 4:15)

a) Utakatifu halisi ni maisha ya kila siku ya kujitakasa mwenyewe kutoka katika dhambi na kutafuta haki.

b) Tafuta utakatifu pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

c) Hatua ya tatu ya Utakatifu ni kugeuzwa kwako na kufananishwa na Kristo kwa utiifu mkamilifu.


II. HATUA MUHIMU ILI KUPATA UTAKATIFU
(2Kor. 7:1)

SAFARI YA UTAKATIFU

1Yoh. 1:7-9
  1. Hatua ya kwanza   Wokovu (kuzaliwa)
  2. Hatua ya pili   Kujitoa (kukua)
  3. Hatua ya tatu    Kugeuzwa (kuimarika)
Hitimisho: Jitoe kikamilifu “Kuwa mtakatifu na ujiunge na wengine waliojitoa kuwa Watakatifu duniani kote”

Ukiwa Mtakatifu lazima Mungu atakuhudumia tofauti na mtu anayejichanganya. Utazijua haki zako na hautaonewa na shetani hata siku moja.
Prepared by; Rev. Joseph Marego Mob: +255754334640/ +255712498080

Thursday, November 15, 2012

TUUTAMBUE MUDA TULIONAO

TUUTAMBUE MUDA TULIONAO
Daniel 9:20-27

Juma 1 = miaka 7
1. (Mstari wa 24) – Majuma 70 ni hesabu ya unabii.

Kwa hesabu yetu juma moja ni sawa na miaka 7.

Kipindi cha miaka 7 kama kuna vipindi 70 na kila kipindi ni miaka 7 tunaweza kuandika hivi 70x7= 490 (miaka).

Majuma 70 (70x7 miaka) inahusu Waisraeli na Yerusalemu – watu wa Daniel na mji wake.

2. (Mstari wa 25) – Tangu kuwekwa amri ya kujengwa upya Yerusalem. Majuma 7 = miaka 49 ilianza na amri ya kujenga na kutengeneza Yerusalem chini ya Ezra na Nehemia. Walijenga hekalu, madhabahu na ukuta.

3. (Mstari wa 26) Majuma 62 = miaka 434 ilianza wakati wa kujenga ukuta wa Yerusalem, kujenga njia kuu na mahandaki (62x7 = 434) na kuendelea mpaka kusulubiwa kwa Kristo.

Mwisho wa majuma 69 unadhihirishia na kutokea kwa Masihi kama mkuu wa Israel.

Masihi anakatiliwa mbali – Kristo anasulubiwa mwishoni mwa Juma la 69.

Kati ya juma la 69 na 70 limeingiliwa na kipindi cha sasa na kanisa. Hii inafanya juma la 70 liwe bado liko mbele.

c. Baada ya miaka 483 (49 + 434) wakati wa maisha ya Taifa la Israel ulisimama.

d. Majira ya Mataifa waanza baada ya juma la 69. Sasa tumo katika kipindi hiki tukingojea kurudi kwa Kristo.

Daniel hakukiona kipindi cha Kanisa.

4. (Mstari wa 27) – mpinga kristo atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma 1(miaka 7).

Juma la 70 = miaka 7 bado haijazaa wakati ambao Mungu atashughulika na Israel peke yake. Huu ni wakati wa dhiki ya Yakobo.

Je! Wewe unajua kuwa muda tayari wa sisi kwenda mbinguni?

 


Prepared by; Rev. Joseph Marego Mob: +255754334640/ +255712498080