Tuesday, October 09, 2012

MAMBO YANAYOSABABISHA KUPOTEZA NGUVU ZA KIROHO/ MUNGU

Mdo. 1:8 – Nitapokea nguvu kutoka kwa Mungu.

Luka 4:1-3

1. Shughuli za kudunia

(Luka 8:14). Hizo zinamfanya mtu ashindwe kumtafuta Mungu kwa maombi na kuabudu. Shughuli za duniani haziishi. Ukilishughulisha nazo ili uzikomoe, zitakukomoa. Hizo ndizo zinazowarudisha watu nyuma.

Zinamsonga mtu anakosa ibada ndani ya moyo wake.

2. kutokutii

a) Neno la Mungu

b) Sauti ya Mungu – inasikika masikioni mwetu

c) Kutii mamlaka (za nyumbani n.k.) (Mwanzo 4:7-9)

3. kujiona bora kuliko wengine

 Mungu akimfanikisha mtu mwengine, anajiona bora zaidi. Mungu hana upendeleo, anawapenda watu wote.

 Katika mafanikio yoyote shetani hukufuatilia ili akuharibie.

 Kinachotakiwa ni kunyenyekea.

4. Kuabudu matatizo

 Yanaweza kukufanya uyaone kama Mungu. Kila unapoenda unawaza matatizo. Muweke Mungu ndani ya moyo wako, siyo matatizo tu.

NB: Mtu akipata mabaya na aombe siyo kuwaza matatizo

i) Neno ni taa

ii) Matatizo ni giza

(Waamuzi 16:15-19)

• Kinachotafutwa ni asili ya nguvu zako.

• Asili ya nguvu zile. Samsoni alipatikana bila kujijua

Shetani anambembeleza mtu aendelee na biashara hadi jioni na kupuuza kwenda kanisani.

Asili ya nguvu zetu ni:

i. Maombi

ii. Kusoma Neno la Mungu

iii. Kuhudhuria ibada

• Usimcheke Samsoni hata na wewe usipokuwa makini unaweza kudanganywa hivyo hivyo.

- Unaweza kulazwa usingizi magotini pa shetani na kuwekwa kwenye shughuli mpaka anakunyoa, kama hupo makini kumtumikia Bwana.

Umelazwa usingizi katika mambo gain?

Labda katika :

Uongo, masengenyo, uvivu, mafanikio, magomvi n.k.

Ukishalala tu, shetani analeta wembe ananyoa:

a) Maombi

b) Utoaji

c) Kuja ibadani

d) Kushuhudia n.k.

Samsoni alikuwa mwanadamu kama sisi.

JIKAGUE UMELAZWA KATIKA MAGOTI YA SHETANI KATIKA LIPI AU KWA NJIA ZIPI?

Angalia ulipolazwa magotini na shetani
 

Prepared by Rev. Joseph Marego.

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed