Wednesday, September 05, 2012

KUWA MAKINI NA WAFANYAKAZI WA NDANI

"WATCH OUT THE DEVIL IS ALL AROUND TO SEEK WHOM HE MAY DEVOUR, AKIKUTA MLANGO UKO WAZI WILL DEFINITELY GET IN (JE WEWE NI MALANGO YAKE AU?) TO DO ALL WHAT HE HAS PLANNED TO DO WITHOUT BEING COUGHT, KESHENI MUOMBE, OMBENI KILA WAKATI BILA KUKOMA. MATHEW 7:7, 1 THES 51-7, 17-18:

GO THROUGH THE STORY NOW AS AM SURE IT WILL CHANGE YOUR LIFE IN ONE WAY OR ANOTHER!

As you may know I have twins Joseph & Magdalene; mimi na familia yangu tunaishi Tabata.

Tulikuwa na wasichana wawili wa kazi na mmoja aliondokaga akabaki mmoja; hivyo tukawa ktk harakati za kutafuta potential replacement ili wawe wawili.

Here comes the story part I.

Jana 21.08.2012 nlipotoka job, wife alinipa taarifa kuwa mdogo wangu wa kike (mwenye salon ya kike kimanga) alimpigia simu kuwa amepata msichana na atakuja nae home jioni akifunga saluni.

Ikabidi nimpigie simu mdogo wangu ili anipe full information.

Mdogo wangu akanimbia majira ya jioni uyo msichana alifika Saluni kwake akidai anatafuta kazi za ndani. Uyo msichana akasema yeye alikuwa anfanya kazi morogoro but ametoroka kwani alikuwa anateswa na mama mwenye nyumba.uyo msichana akizidi kuongeza kuwa yeye hana mawasiliano ya ndugu yeyote ila baba yake anaishi Mwanza but hamjui mama yake. Basi mdogo wangu akamuonea huruma akamkaribisha saluni ilia je nae home jioni na nifanye nae mahojiano ya kina.

Jana majira ya saa 3 usiku baada ya wao kurejea home na kula chakula ikabidi nianze kumhoji yule binti.

Akanitajia jina lake na umri wake 15yrs, na nia yake ni kufanya kazi za ndani na akipata pesa ataenda kwao kusalimia then angerudi tena kuendelea na kazi yake. Ni binti mdogo na nilitamani kumsaidia.

Baada ya kupata maelezo kutoka kwake; nilimuambia kwa sababu hatumfahamu ni lazima tukatoe report kwa balozi/mjumbe kabla hajaenda kulala na alikubali. Nikaenda kwa mjumbe akawa ameshalala; ikabidi nimwambie wife kesho asubuhi (yaani leo) wakiamka waende kwa balozi/mjumbe kutoa taarifa na kuandikishana.

Leo asubuhi najiandaa kwenda kazini; kumbe yule binti ametoroka mapema asubuhi after mlango na geti kufunguliwa. Majirani wakasema walimuona katoka na viatu mkononi wakazani anaenda kutupa taka coz alikuwa anafagiafagia nje. Kuangalia vitu sebuleni na chumbani kwa kina dada ikaonekana everything is OK. Basi nikamwambia mdogo wangu na kijana flani wa jirani wamfuatilie then mimi nikaondoka zangu kuelekea job.

Here comes the story part II.

Majira ya saa 4 asubuhi nikiwa job nilimpigia simu mdogo wangu anitaarifu yaliyojiri:

Akaniambia yule binti walimuona na akakimbilia nursery school flani karibia na Barakuda na kwa msaada wa raia wengine walimkamata. Walimpiga kidogo na kumsachi. Walimkuta na elfu 90 na alikiri kuwa aliziiba katika wallet ya mdogo wangu.

Ikabidi mdogo wangu achukue bodaboda wakaenda nae hadi saluni kwake Kimanga ili akamhoji zaidi. Yule binti akasema kuwa alitudanganya hajatokea Morogoro but anaishi na bibi yake Mbagala na ule ndo mchezo wake yeye na bibi yake.

Akasema kuwa bibi yake ni mchawi na huwa anamtuma kwa nyumba za watu kwa mbinu ya kuomba kazi but baadae wanaiba na kuchukua watoto wadogo kimazingara. Akaongeza kuwa hao watoto wadogo huwa wanawachukua misukule na wengine wakiwa wakubwa wanatumwa kama alivyotumwa yeye.

Yote hayo aliyasema bila woga huku watu wakiwa wamemzunguka pale saluni. Akasema kuwa jana alipoingia getini bibi yake alikuja kimazingara but ghafla macho yake yalianza kumuwasha na hakuwa na amani. Kuona vile bibi ake akaondoka.

Ilipofika muda wa kulala alienda kuoga but aliporudi chumbani alimkuta mdogo wangu anasali ndipo alipigwa na miale ya blue na nyekundu akakimbia kurudi sebuleni. Aliporudi sebuleni alimkuta wife anachek TV nae wife akashtuka kumuona yule binti hana amani.

Baade yule binti akaenda kulala ndipo wife akachukua maji ya Baraka akanyunyiza pale mlangoni na sebuleni kisha akaenda kulala. Yule binti akazidi kuelezea kuwa usiku hakulala kwani aliteseka sana na kuweweseka na bibi ake alipokuja kimazingara hawakuweza kuchukua watoto ikabidi aondoke na kumuacha yule binti kwani alikuwa kaishiwa nguvu. Akasema tangu aanze iyo kazi hajawahi kukamatwa na akmeshangaa sisi tumeweza kumkamata na kueleza siri zake. Akasema bibi yake alimjia kimazingara na akamwambia asirudi kwake kwani ametoa siri. Alionesha chale alizochanjwa na bibi yake kama kinga na alipokuwa anapigwa hakusikia maumivu yoyote.

Alielezea mambo mengi ambayo mdogo wangu hakuweza kunielezea katika simu kwani nae alikuwa anatetemeka kutoamini yaliyokuwa yanatokea. Walimuachia akaondoka zake. I felt so sorry for my twins but I thank GOD wamebaki salama.

Tuwe makini sana na wasichana wa kazi ndugu zangu; you may share it to your relatives and beloved."


By GK
Hii ni email ambayo nimetumiwa na mfanyakazi mwenzangu, ila majina yamebadilishwa kwa ajili ya privacy..

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed