Thursday, July 19, 2012

AJALI YA MV STARGATE AU SKAGIT ZANZIBAR TAREHE 18 JULAI 2012. TUOMBE ROHO YA AJALI ISHINDWE KATIKA NCHI ZETU

MARITIME ACCIDENT IN ZANZIBAR HITS THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA.
Blog yetu ya Tanzania Gospel inaungana na Watanzania kuwapa pole wote waliofikwa na mkasa wa meli ya MV stargate iliyopinduka huko Zanzibar tarehe 19 Julai 2012 . Mungu awape ahueni majeruhi wote. Tukumbuke kuwaombea wote waliopoteza mali, ndugu na jamaa.
Askari wakishirikiana na raia katika harakati za uokoaji katika ajali ya MV Stargate Zanzibar. Watu 100 wanasadikiwa kupoteza maisha katika ajali hiyo. Kutokana na ajali zinazotokea hapa nchini tunatakiwa kuomba sana kuifunga hii roho ya ajali. Meli hiyo ilikuwa na abiria wapatao 280 ambapo abiria 250 walikuwa watu wazima na watoto 30. Watu walionusurika katika ajali hiyo ni abiria wapatao 150.
Prukushani bado zinaendelea huko visiwani Zanzibar ambapo kumegubikwa na wimbi zito la majonzi baada ya meli ya MV Stargate kuzama. Inaelezwa kuwa ajali hiyo ilitokea kwenye kisiwa cha Chumbe kilometa chache kutoka Zanzibar. Meli hiyo ilienda mrama mida ya saa saba mchana na nusu saa baadaye kuzama.
Bado mambo ni magumu huko Zanzibar, ikiwa ni miezi kumi tangu ajali ya spice islanders kutokea. Mzungu mmoja aripotiwa kufa katika ajali ya meli hiyo. Pamoja na kufanya maombi, disaster preparedness ni muhimu sana katika usafiri wa majini. Inafaa kabla ya meli kutoa nanga abiria wafahamishwe kuhusu matumizi ya "life jackets" na maboya ili kupunguza madhara yanayoweza kutokea kwa abiria pindi ajali inapotokea.
Hii ni Google Map inayoonesha Zanzibar ikiwa upande wa kulia wa picha ambapo meli ilizama ambayo ni mali ya mfanyabiashara Saidi Mbuzi. Idara ya hali ya hewa inashauriwa kutoa taarifa za mapema kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Siku meli inazama kulikuwa na upepo mkali sana ambao ulisababisha meli kupinduka katika bahari ya hindi. Kama tahadhari zitakuwa zinatolewa mara kwa mara na idara ya hali ya hewa, tunaweza kudhibiti baadhi ya haya majanga yakiwemo ya mafuriko katika nchi zetu.Kama una habari yeyote hususan inayohusu injili inakaribishwa tuma email: mkahaya@yahoo.co.uk ikiwa na subject "tanzania gospel blog" sms tu: +255717250805. Ubarikiwe!

source: VOA, google,redio,tv,internet n.k.

2 comments:

 1. I wish you had the "google translator" on this so I could read this in English!

  Blessings!

  ReplyDelete
 2. thank you for your advice, but the language is swahili.i can volunteer to teach you swahili till u know it very clearly

  blessings!

  author

  ReplyDelete

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed