Sunday, June 24, 2012

UNAVYOTAKIWA UWE ILI UPOKEE HAJA/ MUUJIZA KUTOKA KWA MUNGU (Zab. 78:41, 42-48)

UTANGULIZI

Usirudi nyuma, halafu ukampa mpaka Mungu aliyetuzaa mara ya pili kwa kuleta wokovu kwa njia ya Yesu Kristo.

I. KOSA KUBWA WALILOLIFANYA
  • Wakarudi nyuma.
  • Wakampa mpaka Mungu.
  • Walisahau matendo na maajabu ambayo Mungu alikuwa ameyatenda kati ya baba yao ambao ni waanzilishi.
Hatupaswi kusahau matendo ya Mungu na miujiza iliyofanywa naye kuanzia A/ Kale hadi A/ Jipya ndani ya watumishi wake waaminifu.

II. JAMBO LA KUFANYA
  • Kuwa na uhusiano mzuri na Mungu.
  • Fanya uamuzi mzuri kubakia kwa kuwa mwaminifu kwa Mungu na kwa Agano lake na Ahadi zake hadi mwisho wako bila kumpa mpaka kwa kila jambo.

 UNATAKIWA:
i. Umwamini Mungu (Mk. 11:22).

ii. Usione shaka moyoni mwako (Mk. 11:23).

iii. Amini umepokea katika uwezo wa Yesu Kristo (Mt. 7:8a, 19:26). Usilolitaka limetoweshwa, tayari halipo tena kwako. Unalolitaka lipo mikononi mwako.

iv. Furahi kama utapata muujiza leo.
Furahi kama hutapata sasa (Flp. 4:4, 11-13)

v. Fahamu kwamba kuchelewa kwa Mungu kujibu maombi yako haimaanishi kukukatalia haja hizo.

Wakati mwingine Mungu analo kusudi kubwa katika mawazo yake kuonyesha utukufu wake (Yoh. 9:3, 11:4, 2Kor. 12:7-10)."TAMBUA KWAMBA KAMA WEWE UMEJITOA KIKAMILIFU" MUNGU HAWEZI KUKUACHA WALA KUKUSAHAU, ANAKUPENDA MNO KIASI KWAMBA AMEKUCHORA KATIKA VIGANJA VYA VYA MIKONO YAKE (Isa. 49:15-16, Zab. 121:1-2).


Imetayarishwa na
Rev. Joseph Marego.
Mob: +255754334640, 255712498080

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed