Saturday, June 23, 2012

SIFA ZA WEMA WA MUNGU (Zab. 139:7-8)


UTANGULIZI

Tabia nyingi za Mungu wa kweli na hasa sifa, za wema wake zinafanana na za mwanadamu. Hata hivyo sifa zake zipo katika kiwango cha juu kuliko ilivyo kwetu.

Isisitizwe kwamba uwezo wetu wa kuweka katika matendo tabia hizi unahusiana na kuwa kwamba sisi tumeumbwa tatika mfano wa Mungu (Mzo. 1:26-27) kwa maeneo mengine, sisi tuko kama yeye na siyo yeye kama sisi.

1.Mungu ni mwema (Zab. 25:8, 106:1 Mk. 10:18) yote yaliyokuwa yameumbwa na Mungu tangu mwanzo yalikuwa mema, maendelezo ya asili yake mwenyewe. (Mzo. 1:4, 10, 12, 18, 21, 31). Anaendelea kuwa mwema katika uumbaji wake kwa kuutegemeza kwa niaba ya viumbe wake wengine wote (Zab 104:10-28, 145:9).

NB: Mungu ni mwema hasa kwa watu wake wamwitapo katika kweli (Zab. 145: 18-20)

2.Mungu ni upendo (1Yoh. 4:8). Upendo wake hauna ubinafsi ni upendo unaokumbatia dunia nzima ya mwanadamu mwenye dhambi (Yoh. 3:16, Rum. 5:8). Udhihirisho unaonekana kumtuma mwanaye pekee Yesu kuwafia wenye dhambi (1Yoh. 4:9-10).

3.Mungu ni wa huruma (2Fal. 13:23, Zab. 86:15, 111:4)

Kuwa na huruma maana yake ni kusikitika kwa makosa ya mtu mwingine apatayo, na kuwa na shauku ya kumsaidia.
Katika huruma yake kwa mwanadamu, Mungu anatoa msamaha na wokovu (Zab. 78:38).

Tahadhari: Hata hivyo uumilivu wa Mungu na msamaha visitumiwe vibaya, kwa kutotii kwa kudhamiria na kuasi. Kama tutaendelea kumhuzunisha kwa dhambi zetu, hatimaye atatuhukumu kwa ghadhabu yake kama alivyofanya kwa Israel (Ebr. 3:7-19).


4.Mungu ni mvumilivu na siyo mwepesi wa hasira (Kut. 34:6, Hes. 14:18, Rum. 2:4, 1Tim. 1:16).

Mungu kwa mara ya kwanza alionesha tabia yake katika bustani ya Edeni, baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi. Alikuwa na haki ya kukiharibu kizazi cha mwanadamu, lakini hakufanya hivyo (Mzo. 2: 16-17)

Mungu pia alikuwa mvumilivu katika siku za Nuhu wakati safina ilikuwa imejengwa (1Pet. 3:20). Bado Mungu anakivumilia kizazi chenye dhambi cha mwanadamu. Hatoi hukumu sasa hivi ya kuiangamiza dunia, kwasababu anangoja kwa uvumilivu ili kumpa kila mtu nafasi ya kutubu na kuokolewa (2Pet. 3:9).
5.Mungu ni mkweli (Kumb. 32:4, Zab. 31:5, Isa. 65:16, Yoh. 3:33)

Yesu alijiita mwenyewe ''kweli'' (Yoh. 14:6) na Roho anajulikana kama Roho wa kweli (Yoh. 14:17).

6.Mungu ni mwaminifu (Kut. 34:6, 7:9 Isa. 49:7, Ebr. 10:23).

Mungu hufanya yale yaliyofunuliwa katika Neno lake, ahadi zake na tahadhari (Hes. 14:32-33, 2Sam. 7:28, Ay.34:12, Mdo. 13:23, 32-33)

Uaminifu wa Mungu unaleta faraja kubwa kwa waumini

...................................................................inaendelea......................................................

Imetayarishwa na

Rev. Joseph Marego.

Mob: +255754334640, 255712498080 email: mkahaya@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed