Wednesday, May 02, 2012

PROXIMITY IS IMPORTANT BETWEEN CHRISTIAN COUPLES | UKARIBU NI MUHIMU KATI YA WANANDOA WAKRISTO


For comments or questions mkahaya@yahoo.co.uk only send SMS to +255717250805

Kwa maoni au maswali mkahaya@yahoo.co.uk tuma sms tu +255717250805

Pastor Chris and Anitha Oyakhilome

By Our Correspondent, Festus .
Last week we talked about closeness in relationships between couples who are saved and accept the Lord Jesus as the leader and the saviour of life. We talked about many things that we see as small but highly significant in improving relations between the couple. Today we conclude our study by describing other matters that can be a source of catalyst of love between the couple who saved.

we will discuss whole issue of transparency in the area of income and avoiding selfishness. Many men and women are not open on the whole question of income and this leads to them lacking the freedom to get something that they needed. For example there are many cases (we refer to characters) where the woman asks money from her husband's when they are outside the house. Sometimes a woman dared to send his son, who sees much loved by her husband and ask his father for spending money. Spending is something that the wife and her husband should sit and discuss at their own bedroom. When you get out of the room all matters have to be clear. Children should only participate in choosing food that they would need to eat for the day. But in the process of budgeting father and mother play the primary role.

Also, can see that men have a hard time when they were without anything due to factors such dismissal or leaving their own jobs and many other factors.

You can see when the man needs something that could help him in everyday life such as clothes. The man is unable to ask his wife simply because he is afraid of being embarrassed. Beloved let us stop this behavior if the wife has something, it is your responsibility to sit down together to plan expenditure together by considering relevant income limits.

The issue of selfishness dominated among the hearts of many couples. For example you can see the couple live together when they are all employees and all receive good income. But due to the selfishness you see one of the couple spending the money alone for pleasures and private activities; this is seen by most men. For women you can see that they spend money of their husbands in various activities and when they see any need at home they lay the whole load to them (their husbands) .however, they do other activities different from the development of their family. These women can spend their money on such things as building the houses in their village even though she and her husband don’t have a house.

getting rid of various problems in relationships couples are required to be clear in terms of revenue and avoid selfishness. Also, couples are advised to be very close in issues that are potential in marriage as well as knowing what one spouse likes and dislikes and other related matters. Fearing God and being faithful are enough weapons towards a better and successful marriage.


UKARIBU NI MUHIMU KATI YA WANANDOA WAKRISTO

Kwa maoni au maswali mkahaya@yahoo.co.uk tuma sms tu +255717250805

Wiki iliyopita tulizungumzia sana kuhusu kuwa na ukaribu katika mahusiano baina ya wanandoa waliookoka na kumkubali Bwana Yesu kuwa ndiye kiongozi na tegemeo la maisha yao. Tulizungumzia mambo mengi ambayo tunaona kuwa ni madogo lakini yenye umuhimu mkubwa katika kuboresha mahusiano baina ya wanandoa.

Leo tutamalizia somo letu kwa kueleza mambo mengineyo amabayo yanaweza kuwa chanzo cha chachandu ya upendo baina aya wanandoa waliookoka.

Nitaongeelea suala zima la uwazi katiak mapato na kuepuka ubinafsi. Wanaume na wanawake wengi siyo wawazi katiaka suala zima la mapato na hii husababisha wanawake na wanaume wengi kukosa uhuru wa kupata matumizi pindi pale wanapohitaji. Kwa mfano kuna kesi nyingi (wahusika hatuwataji) ambapo mwanamke humwomba pesa ya matumizi mume wake wakati wakiwa wameshatoka nje. Mara nyingine mwanamke hudiriki hata kumtuma mtoto wake anayeona anapendwa sana na mmewe akamwombe babake pesa ya matumizi. Suala la matumizi ni kitu ambacho mke na mmewe wanatakiwa kukaa chumbani na kujadili kwanza wenyewe. Wanapotoka nje ya chumba mambo yote yawe yameshawekwa bayana. Watoto wanatakiwa tu washirikishwa kuhusu chakula abacho wangehitaji kula kwa siku hiyo. Lakini katika mchakato mzima wa kapanga matumizi baba na mama ndiyo wenye jukumu la msingi.

Vile vile unaweza kuona kuwa wanaume wanapata wakati mgumu pale wanapokuwa hawana kitu kutokana na sababu kama kuachishwa kazi ama kuacha wenyewe kwa ridhaa yao na sababu nyingine nyingi.

Unaweza kumwona mwanaume akiwa anahitaji kitu cha msingi ambacho kingemsaidia katika maisha ya kila siku kwa mfano nguo ya ndani. Mwanaume huyu hushindwa kuifikisha hoja yake kwa mkewe akiogopa eti kile kinachitwa kujidhalilisha. Wapendwa tuache tabia hii kama mke ana kitu,ni jukumu lenu pamoja kukaa chini kupanga matumizi kwa pamoja huku yakizingatiwa yale mahitaja ya muhimu na ya pamoja ambayo mmoja wa wanandoa anayo kwa wakati husika kwa kuzingatia kipato kilichopo.

Suala la ubinafsi limejaa na kusheheni miongoni mwa mioyo ya wanandoa wengi. Kwa mfano unaweza kuwaona wanandoa wawili wanaishi pamoja wakiwa wote ni waajiriwa na wote wanapokea kipato kizuri tu. Lakini kutokana na ubinafsi utamwona mmoja wa wanandoa anatumia fedha peke yake kwa shughuli za anasa na kusahau watu wa famillia yake, hii huonekana kwa wanaume walio wengi. Kwa wanawake unaweza kuona kwamba wanatumia tu pesa za waume zao katika shughulu mbalimbali na pale wanapoona kuna hitaji lolote nyumbani huwaelemea mzigo wote waume zao wakati pesa zao zikiwa zinafanya shughuli nyingine tofauti na maendeleo ya familia yao. Wanawake hawa huweza kutumia hizo pesa zao kwa mambo kama kujenga nyumbani kwao hata kama yeye na mmewe bado hawana nyumba na kuwahonga vijana wadogo almaarufu ‘serengeti boys’ jina linalotumiwa Tanzania.

Kuepuka matatizo mbalimbali katika mahusiano baina ya wanandoa kinachohitajika ni kuwa mwazi kimapato na kuepuka ubinafsi pamoja. Pia, wanandoa wanashauriwa kufahamiana kuindani katika mambo yanayoleta tija katika ndoa kama vile kufahamu kitu mwanandoa mmojawapo anachopenda na mambo mengineyo. Kumtegemea Mungu na kuwa waaminifu ni silaha tosha katika kuwa na ndoa bora na iliyofanikiwa.

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed