Friday, May 11, 2012

FAHAMU JINSI INAVYOPASA KUJILINDA KATIKA MAISHA YA WOKOVU. Ebr. 2:3 BY REV. JOSEPH MAREGO

Mchungaji Marego (kulia) akiwa na mkewe (kushoto) katika picha.

1.KUJALI-Ni kuchukua tahadhari,tia maanani, sikiliza,heshimu.

2.MAENEO HATARI KWA MAISHA YAKO KUYADHIBITI: 
 i. Moyo:
Moyo ni eneo muhimu sana katika maisha yako;inakupasa uwe mwangalifu. Asili ya moyo ni kwamba ni mdanganyifu. Moyo una siri kubwa sana unalinganishwa na nyumba. (Yeremia 17:9-10, Luka 21:34-36)

Uuulinde sana (Mith 4:23)hili ni eneo la tahadhari

ii. Kinywa na ulimi:

•Hii pia ni sehemu muhimu sana ambayo inapaswa kudhibitiwa kwa umakini sana.

1.Daudi-aliomba awekewe ulinzi kinywani pake.(Zab 141:3-4)

2.Isaya- alitambua yeye yupo katikati ya watu wenye kusemasema ovyo.(Isaya 6:5-7)

3.Sulemani -alitambua juu ya kukilinda kinywa (Mith 13: 1-3)

4.Yakobo -alitambua kutofugika ulimi (Yak 3:8-12 )

•UWE NA SIFA HIZI: (Zab 71:8, 15, 23-24)

iii. Macho:

Macho yako yasiwe na makengeza ya kiroho. (Mith 4:25-27)

Macho ni kiungo cha hatari chenye tabia ya wizi

Yakobo 4:7-10- Mtii MUNGU 100%
 
 


Imetayarishwa na: Rev. Joseph Marego. Senior Pastor, Kimanga E.A.G.T. Dar es Salaam, TANZANIA. Mob. No:+255655334640,+255714263144. Email; mkahaya@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed